Jumapili, 27 Aprili 2014 05:10

Joomla! imewezesha Kiswahili kutumika katika wavuti wote

Written by
Rate this item
(0 votes)

Swahili (kiswahili) ni lugha ya taifa katika nchi tano: Tanzania, Kenya, Congo (DR), Comoros na Uganda na pia Rwanda, pia inatumika kaskazini Mozambique, Burundi, Malawi na kusini Sudan. Na inakadiriwa na ratiba kama milioni nne ya watu wanaongea kiswahili kama lugha yao ya asili, na kwa ujumla ya watu milioni miamoja wanaongea kiswahili.

Kwa jina la waswahili wote kutoka ulimwengu mzima wanampongeza JM (ni mmojawapo ya watu walio buni Joomla!) kwa uamuzi wake bora kwa kuchagua jina la Jooomla! Kutoka kwa lugha ya kiswahili. Kulikua na aibu kubwa sana kwa waswahili wote, hata kama jina la Jomla! linatokana na lugha ya kiswahili, kwa muda mrefu sana lugha ya kiswahili haikuweza kutumika kwa Joomla! mpaka Hassan (Ayeko) alipochukua uwamuzi wa kujitolea kufanya kazi hii pekeake, na mpaka leo kila mtumiaji wa joomla anaweza kutumia kiswahilli kutokana na kazi ya Hassan aliofanya.

Ingawa kuna nambari kadhaa za swahili dialects, iliamuliwa kuwa ni lugha moja pekee ikusanywe kwa Joomla! Ili kupunguza kazi nzito kwa usasishaji wa kila toleo jipya la Joomla! .

Tuko nania ya kutumia lugha moja rasmi 'juu ya Swahili, na tunawania kutumia fomu ya Swahili ambayo inaweza kuweka kiwango kimoja na kueleweka Afrika Mashariki nzima. Tofauti kati ya dialects, ambazo zinajulikana kwa siku za maisha, ni ndogo sana na tukija kwa upande wa teniki wa lugha inayotumika kwa Joomla!

Kwa muda wasasa tunatumia codi ya lugha ya kiswahili ni sw-KE, kwa sababu hakuna codi ya lugha ya Afrika Mashariki. Kwa hivyo fungu la lugha linakuja na bendera ya Umoja wa Afrika Mashariki kuonyesha kwamba inatumika kwa Afrika Mashriki nzima na ni lugha moja pekee kwa africa mashariki nzima.

Lugha ya kiswahili kwa sasa hivi iko kwa Joomla! toleo 2.5.10 na 3.1.0 na itasasishwa kwa kila toleo jipya.

Hassan Ayeko

Hassan ni mtaalamu wa masuala ya IT pia ni mkalimani mkuu wa Joomla Kiswahili (Joomla Coordinator for Swahili language)

www.att-center.de