Tovuti hii ya Joomla Afrika Mashariki imeanzishwa ili kuwapatia jukwaa la majadiliano, elimu na maarifa juu ya Joomla kwa watumiaji wake kutoka ukanda huu. Neno Joomla! limetokana na neno la Kiswahili "Jumla" hivyo kuna umuhimu sisi kama watumiaji wa Kiswahili kuikumbatia Joomla, kwa kufanya hivi, sio tu tutaweza kuonyesha umuhimu wake, bali pia itatuwezesha kuifahamu joomla ipasavyo tutaweza kupiga hatua kwenye matumizi yake ipasavyo.

Jukwaa hili sio tu litaweza kuwaunganisha watumiaji wa Joomla kwa kiswahili, bali pia litaweza kutoa nafasi kwa watumiaji wake kubadilishana ujuzi, maarifa pamoja na dhana mbalimbali zitumikazo kwenye Joomla.

Ndani ya Tovuti ya Joomla Africa Mashariki, utaweza kujifunza kwa njia ya Video, Makala mbalimbali toka kwa waandishi waliobobea kwenye matumizi ya Joomla pia utaweza kujadiliana na watumiaji wenza kwenye jukwaa la majadiliano.

Waanzilishi wa Joomla Afrika Mashariki ni Hassan Abdalla (Ayeko) na Ngaranyiza, ambao wote ni watumiaji wa Joomla kwa miaka kadhaa. Joomla ndio iliyowakutanisha Ngaranyiza na Hassan na kwa kuona umuhimu wake kwa Jamii ya Afrika ya Mashariki ndio wakaja na wao hili la kuanzisha jumuiya hii. Ngaranyiza akitokea Tanzania na Hassan akitokea Kenya sehemu ambazo Kiswahili ni lugha ya Taifa, ni dhahiri kuwa sasa milango imefunguka kwa watumiaji wa Joomla.

Hassan ni Mratibu wa Joomla katika lugha ya Kiswahili (Swahili Language Coordinator for Joomla). Kulikuwa na majaribio mengi ya kutafsiri au (kufanya Joomla!). Iliiwezekupatikana katika lugha ya Kiswahili, lakini wao walikuwa mara wanase watatengeza wakati fulani au hakuna maneno ya kiswahili. Kwa hivyo ndio mwisho Hassan aliamua kuchukua hatua juu ya kazi yake na kutafsiri mfumo nzima wa Joomla kwa Kiswahili na pia ametengeza maneno yeyemwenyewe kwavile yeye pia ni mtaalamu wa malugha na upande wa uinjinia. Yaani mtaalamu wa computa, mifumo na matovuti. Na sasa matoleo ya lugha ya kiswahili yanapatikana ni 2.5 na 3.x.

Hassan alizaliwa na kukulia katika mji wa Mombasa, Kenya na sasa anaishi Schweinfurt, Ujerumani

Ngaranyiza alizaliwa na kukulia katika mji wa Tanga, Tanzania.

Kushiriki:

Katika kuhakikisha tunapanua wigo wa matumizi ya Joomla katika Afrika ya Mashariki, tungependa kukaribisha watu wengi zaidi wenye ari na moyo wa kujitolea kutumia ujuzi wao katika kuelimisha jamii kujiunga na timu yetu ya waandishi wa makala, viranja wa midahalo (Forums Moderators) na pia wakufunzi kwa njia ya video. Tuandikie kwenye Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. ukifafanua ni wapi ungependa kushiriki.

Ni mategemeo yetu kuwa Jukwaa hili litakuwa na manufaa kwa Jamii nzima.

Uongozi

Joomla Afrika Mashariki