Sababu kubwa inawezekana ni kutokana na hofu ya kuhamia Joomla 2.5 kwani kuhama toka Joomla 1.5 kwenda 2.5 ni kama kuhamisha wavuti nzima hivyo wamiliki wengi wa wavuti wameona bora nusu shari kuliko shari kamili hivyo wameamua kubaki kwenye Joomla 1.5, ila mimi nasikitika kukutaarifu kuwa hiyo ni dharuba, bora masika kuliko Tsunami.
Kwakuwa hakuna tena masasisho kwenye Joomla 1.5 , hivyo basi inakabiliwa na vihatarisho lukuki. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema, upo kwenye hatari.
Ili kuwasaidia wamiliki ambao bado wanafikiria ama waende Joomla 2.5 ama wabaki kwenye Joomla 1.5, fuatilia mchoro wa chini.
Pia unaweza kuishusha picha hii kwa kwenda Hapa.