Jumatatu, 21 Aprili 2014 23:20

Faida za kuwa na wavuti kwa biashara yako

Written by

Kwa mara kadhaa nimekuwa nikiongea na watu wengi juu ya suala la kuwa na wavuti ya biashara zao. Wengi wakisema kuna umuhimu gani kwani hata sina uhakika kama kuna mtu atatembelea. Pia wengi wa wafanyabiashara hawa wana mambo mengi sana hivyo kwa wao hakuna muda wa kwa ajili ya wavuti, kwa wao husema wavuti ni kitu cha ziada.

Kulingana na matokeo ya tafiti kutoka internetworldstats zinaonesha kuwa, kwa mwaka 2012, watumiaji wa internet kwa Tanzania walikuwa 11% ya Watanzania wote, hii inamaanisha kwa katika kila Watanzania 10, angalau mmoja anatumia internet.Huu ni muongezeko wa mkubwa ukilinganisha na watumiaji 1.6% mwaka 2005. Matokeo haya yanaashiria ongezeko kubwa la watumiaji siku hadi siku.

Jumanne, 01 Aprili 2014 05:23

Joomla 3.2.x inapatikana sasa

Written by

Usakinishaji ni rahisi sana. Ni kuingia tu upande wa nyuma wa msimamizi (administrator side) katika tovuti yako na kubofya kibonyezo cha sakinisha. Vinginevyo, na unaweza kushusha kamili au kusakinisha paketi kutoka kwa tovuti ya Joomla kama ilivyoelezwa hapo chini. Unashauriwa kusoma maelezo ya toleo kwanza. Ilani na unashauriwa kufanya backup ya wavuti wako kabla ya kwenda kwa toleo jipya. Kwa uboresho wa matoleo ya awali, angalia ilani hapo chini.

Jumatatu, 31 Machi 2014 08:22

Mavutio katika Jukwa la Joomla!

Written by

Ni vipi nitashusha Joomla?

Ni rahisi kushusha Joomla! Nenda tu kwa joomla.org na bofya kibonyezo cha kushusha.

Ni nini baadhi ya uwezo wa Joomla?

Usimamizi wa watumiaji - Joomla ina mfumo wa kusajili ambao utaruhusu watumiaji kusanidi machaguo yao ya kibinafsi.

Ijumaa, 14 Machi 2014 07:20

Mazingatio juu ya kuchagua wapi pa kuweka tovuti

Written by

Katika miaka ya tisini,tovuti ilikuwa ni kwa ajili ya kusomea barua pepe,kipindi hicho ukiwa na barua pepe basi wewe unaonekana ni bingwa na mtaalam.Maendeleo hayo ya tovuti kwa nyumbani yaliendelea kuwa ni anasa mpaka miaka ya karibuni ambako kwa kasi ya ajabu mambo yamebadilika na kubadilisha uelekeo wa upepo. Ili kuweka mambo sawa zaidi,tuifananaishe tovuti na nyumba,kwani ndani ya tovuti ndipo hazina yako inapokaa kama sisi tunavyokaa kwenye nyumba,unapozungumzia nyumba,kuna makundi mengi,kuna wale wenye nyumba binafsi na wale walioamua kupanga,tovuti nayo vilevile. Leo hii nitakufafanulia kwa undani ni mambo gani unatakiwa kuzingatia kipindi unachagua wapi pa kuweka hazina yako,tutaangalia sana kikazi na kukufanya ujue nini unatakiwa kufahamu ili kuhakikisha unakuwa na tovuti imara na isiyosumbua au kukutia aibu.

Najua wengi watakuwa wapo excited mno na kutengeneza tovuti zao, ni kweli joomla inarahisisha mambo na kufanya kazi nzima ya utengenezaji wa tovuti kuwa rahisi zaidi. Ila ukweli ni kuwa bado kuna mengi yanatakiwa kufanyika baada ya kutengeneza hiyo tovuti.

Chukulia wewe ni mtengenezaji wa tovuti, baada ya kumaliza kutengeneza tovuti na kumkabidhi mteja wako, wengi wa hawa wateja huwa hawana ufahamu mkubwa wa hii joomla hivyo hufanya mambo mengi mno na kuifanya ile tovuti ambayo wewe ulitengeneza na kujigamba nayo kuwa kimeo na hata kukufanya uikane kama wewe ndiye uliyetengeza. Hii ni kwa sababu wengi wa wanaoanza au kutokuwa na uzoefu wa joomla hufanya makosa mengi kwenye tovuti, hivyo leo nitazungumzia makosa matano ambayo watu hufanya kwenye tovuti za joomla.

Unaweza kusema je Joomla ni kimeo, ukweli ni kuwa, sio kimeo ila urahisi wake unaweza kuwafanya watu wafanye makosa mbalimbali!

Makosa haya ni kutokana na uzoefu wangu binafsi ambao niimepitia hadi kufika hapa nilipo:

Ukurasa 3 ya 4