Ngaranyiza

Ngaranyiza

Mtumizi wa Joomla! myaka mingi iliopita

Unataka kujua vitendo gani vya utawala vimefanyika kwenye tovuti yako? Shukrani kwa Joomla 3.9, Watumiaji Wapya wanaweza kuona urahisi mtumiaji gani alifanya, na wakati gani. Na pia inafanya kazi na upanuzi wa mkono! Kagua batli ya kitendo, uifirishe na uondoe funguo. Hutakosa hila, kwa shukrani kwa moduli za vitendo vya hivi karibuni ambavyo vinaweza kuongezwa kwenye paneli yako la kudhibiti.
Unahitaji zaidi? Kisha uwezeshe Plugin mpya ya mzunguko wa batli - hii itawawezesha kuzunguka na kuondoa faili zako za batli.

Unahitaji watumiaji kukubali sera yako ya faragha na / au masharti na hali? Na Joomla 3.9, yote yanatunzwa moja kwa moja. Fanya na kuunda fomu yako ya msingi kwa urahisi na kuomba idhini kabla ya kukusanya data yoyote ya kibinafsi.
Unaweza pia kuanzisha muda wa ridhaa ya ridhaa ya faragha. Mfumo utawajulisha ikiwa na wakati unahitaji kuwasiliana na watumiaji wako ili upate idhini.
Ufuatiliaji wa watumiaji wa ufuatiliaji, udhibiti mabadiliko ya sera ya tovuti na mengi zaidi, yote, na mtazamo kwenye dashibodi yako.

Jumatatu, 21 Aprili 2014 23:20

Faida za kuwa na wavuti kwa biashara yako

Kwa mara kadhaa nimekuwa nikiongea na watu wengi juu ya suala la kuwa na wavuti ya biashara zao. Wengi wakisema kuna umuhimu gani kwani hata sina uhakika kama kuna mtu atatembelea. Pia wengi wa wafanyabiashara hawa wana mambo mengi sana hivyo kwa wao hakuna muda wa kwa ajili ya wavuti, kwa wao husema wavuti ni kitu cha ziada.

Kulingana na matokeo ya tafiti kutoka internetworldstats zinaonesha kuwa, kwa mwaka 2012, watumiaji wa internet kwa Tanzania walikuwa 11% ya Watanzania wote, hii inamaanisha kwa katika kila Watanzania 10, angalau mmoja anatumia internet.Huu ni muongezeko wa mkubwa ukilinganisha na watumiaji 1.6% mwaka 2005. Matokeo haya yanaashiria ongezeko kubwa la watumiaji siku hadi siku.

Katika miaka ya tisini,tovuti ilikuwa ni kwa ajili ya kusomea barua pepe,kipindi hicho ukiwa na barua pepe basi wewe unaonekana ni bingwa na mtaalam.Maendeleo hayo ya tovuti kwa nyumbani yaliendelea kuwa ni anasa mpaka miaka ya karibuni ambako kwa kasi ya ajabu mambo yamebadilika na kubadilisha uelekeo wa upepo. Ili kuweka mambo sawa zaidi,tuifananaishe tovuti na nyumba,kwani ndani ya tovuti ndipo hazina yako inapokaa kama sisi tunavyokaa kwenye nyumba,unapozungumzia nyumba,kuna makundi mengi,kuna wale wenye nyumba binafsi na wale walioamua kupanga,tovuti nayo vilevile. Leo hii nitakufafanulia kwa undani ni mambo gani unatakiwa kuzingatia kipindi unachagua wapi pa kuweka hazina yako,tutaangalia sana kikazi na kukufanya ujue nini unatakiwa kufahamu ili kuhakikisha unakuwa na tovuti imara na isiyosumbua au kukutia aibu.

Siku si nyinzi zilizopita tumeanza kutoa mafundisho ya matumizi ya joomla, ni dhahiri kuna watu wengi wamepata na mori na kuanza kutumia joomla. Pia jana katika pitapita zangu tena katika tovuti moja ya idara muhimu ya serikali nikaona kuna matangazo ya ajabu mno ya video za kikubwa (hehe), hii ilifanyika bila webmaster kujua. Hivyo ili kuwasaidia mawebmaster wanaoanza, leo hii tuangalie mambo machache ambayo wewe kama webmaster wa joomla unatakiwa kuzingatia. Kumbuka haya ni mazingatio muhimu ambayo unatakiwa kuzingatia kabla ya kuweka tovuti yako online.

 

 

Najua wengi watakuwa wapo excited mno na kutengeneza tovuti zao, ni kweli joomla inarahisisha mambo na kufanya kazi nzima ya utengenezaji wa tovuti kuwa rahisi zaidi. Ila ukweli ni kuwa bado kuna mengi yanatakiwa kufanyika baada ya kutengeneza hiyo tovuti.

Chukulia wewe ni mtengenezaji wa tovuti, baada ya kumaliza kutengeneza tovuti na kumkabidhi mteja wako, wengi wa hawa wateja huwa hawana ufahamu mkubwa wa hii joomla hivyo hufanya mambo mengi mno na kuifanya ile tovuti ambayo wewe ulitengeneza na kujigamba nayo kuwa kimeo na hata kukufanya uikane kama wewe ndiye uliyetengeza. Hii ni kwa sababu wengi wa wanaoanza au kutokuwa na uzoefu wa joomla hufanya makosa mengi kwenye tovuti, hivyo leo nitazungumzia makosa matano ambayo watu hufanya kwenye tovuti za joomla.

Unaweza kusema je Joomla ni kimeo, ukweli ni kuwa, sio kimeo ila urahisi wake unaweza kuwafanya watu wafanye makosa mbalimbali!

Makosa haya ni kutokana na uzoefu wangu binafsi ambao niimepitia hadi kufika hapa nilipo: