Siku za karibuni tumeshuhudia kwa wafanyabiashara wachache waliopata muamko kuanza kutumia blogs kama njia mojawapo za kuingia online. Hii inawezekana na sababu ya urahisi wake au kukosa motisha na nguvu ya kuwafanya wawe na tovuti kamili. Lakini, swali la kujiuliza, ni kwanini wengi wa hawa wafanyabiashara wamekuwa wagumu kutumia wavuto kamali kama sehemu ya biashara zao? Leo hii haishangazi kuona mmiliki wa hoteli kubwa anakupa kadi yake ina Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.. Je ni kwa sababu hawafanamu umuhimu wa kuwa na tovuti kamili au kuna vikwazo vinavyowafanya wakate tamaa juu ya malengo ya kuwa na tovuti?
Hebu tuangalie faida zitokanazo na kuwa na wavuti ya kampuni
1. Kuwafikia watu wengi zaidi.
Kama tulivyoona, kwenye watu kumi, mmoja anatumia internet, je hutaki kuwa wa kwanza kumshawishi huyo mtu mmoja atumia biashara yako? Kwa kuwa na wavuti utawafikia sio tu wale walio karibu yako, balo pia hata watu walio maili elfu na elfu.
2. Kuvutia wateja makini
Chukulia mfano wewe una duka la nguo, wateja wengi wangependa kupata taarifa juu ya mzigo mpya, mapunguzo nk bila hata kuja dukani kwako. Kwa kuwa na wavuti, ni dhahiri utavutia sana wateja makini ambao hupenda kupata taarifa za kina kabla ya kununua bidhaa. Wavuti inakupa wasaa wa kujieleza kwa undani juu ya huduma au bidhaa zako.
3. Kujenga uhusiano wa karibu na wateja.
Je umewahi kujiuliza, ni wateja wangapi ambao huwa marafiki zako baada ya kutumia / kununua bidhaa yako? Je unatumia njia zipi kudumisha uhusiano kati ya mteja na mtoa huduma? Wanazuoni husema, biashara itakayodumu ni ile tu iliyofanikiwa kujenga uhusiano mzuri na wateja wake. Kwa kuwa na wavuti, sio tu utaweza kupata maejesho juu ya ubora wa huduma yako, bali pia utaweza kudumisha mawasiliano kati yako na mteja, kumbuka mawasiliano ndio hudumisha uhusiano.
4. Kufanya biashara moja kwa moja.
Katika dokezo lango moja kwenye Facebook, niliwahi kuandika " Goodbye IT, welcome Digital Business", wengi hawkuelewa nini nilimaanisha hadi pale nilipokuja kufafanua, na kuna waliochanganya na hii huu mfumo wa digitali. Kwenye makala hii niliposema Digital Business nilimaanisha kutumia IT kama biashara ndio tunachokiita digital business.
Ukweli ni kuwa, Watanzania wengi wamekuwa wagumu na bado hawaamini kama kuna uwezekano wa kufanya biashara moja kwa moja online. Hii inawezekana ni kutokana na kasumba yetu ya kuogopa kuanza hadi pale tunapoona mtu amefanikiwa.
Ukweli ni kwamba, tunaweza kuuza na kununua moja kwa moja online, tena ukizingatia Tanzana ni nchi yenye watumiaji wengi wa simu za mkononi ambazo pia huwawezesha watu kulipia kwa kuhamisha pesa. Hivyo kwa kutumia huduma hizi, unaweza kufanya bishara moja kwa moja. Chukulia mfano wamiliki wa migahawa, maduka ya urembo nk. Wavuti inaweza kuwasaidia watu hawa kupanua na kuboresha wigo wa huduma zao.
Sasa, ingawa kuna faida nyingi kama hizi, je ni kwanini wengi wamekuwa waoga au hawapo tayari kutumia huduma hizi? Hebu tuangalie sababu za kawaida (Zisizo za kiufundi )
1. Gharama za kutengeneza tovuti ni kubwa kulinganisha na faida yake.
Kama inavyofahamika, kwenye biashara yoyote hakuna kitu kinachoitwa ninafanaya ili na mimi nionekanae, bali kila kitu lazima kiwe na rejesho la faida, ama iwe ya moja kwa moja au baadae. Katika ulimwengiu wa IT, hakuna kitu kigumu kama kupima faida za IT kwa biashara, haswaa kwa wale wanaotumia IT kama nyenzo na si sehemu ya kazi.
Hivyo, utaona kuwa kwa wale ambao hawapo kwenye digital business (kama nilivyodokeza hapo juu),ni ngumu kuona faida za IT, hii ni kwa sababu faina nyingi za IT si za moja kwa moja. Kwa mfano, kwakuwa na wavuti na barua pepe rasmi itakusababishia watu wengi wakuamini na kuridhia kufanya biashara na wewe. Hivyo ni kwa wafanya biashara wachache mno wanaoweza kufuatilia muonendo wa biashara zao kitu na kubaini faida iliyoletwa na IT.
Hivyo hii ni sababu kubwa kwa wengi kutupa wazo la kuwa na wavuti.
2. Elimu haba juu ya Wavuti.
Nilipomaliza kutengeneza tovuti na programu ya idara moja kubwa ya serikali, nilipata nafasi ya kuwapa darasa juu ya matumizi yake. Siku ile wengi waliingia mitini wakisema mimi nimeshazeeka kuanza kujifunza kompyuta. Wengi bado wanaamini kuwa na wavuti ni darasa lingine la kompyuta, hivyo huingiwa na ganzi kwa kuhofia kutoweza kufikia malengo.
Leo hii ukienda google na kutafuta maarifa yoyote kwa kiswahili, utabofya hadi vidole viote kutu. Hii ni kwa sababu Watanzania wenye ufahamu wa mambo wamekuwa wagumu mno kuandika makala za fani zao. Wengi wamejikita kwenye habari, habari na habari kwa kwenda mbele. Hii huwafanya watu wasio na ufahamu kukosa sehemu pa kujifunzia, angalau vitu vya msingi.
3. Kasumba za wana IT wa Kitanzania.
Mwezi ulipita nilikuwa ninamfundisha mmoja wa mtu wangu wa karibu masuala ya tovuti, tulikuwa tunafanya wote baadhi ya project kuanzia mwanzo hadi mwisho. Biinafsi, huwa ninapenda jambo la leo liishe leo hivyo kuna wakati nilikuwa ninamaliza project ndani ya siku moja. Kuna siku aliniambia,"Nyoni huwezi kumaliza hii kai kwa siku moja, mteja atakuona haujafanya kitu".Hivyo chukua muda angalau siku mbili tatu ili ulete ladha kwenye utendaji wako. Hii inadhihirisha kuwa, wana IT wengi wamekuwa na kasumba kuwa ukifanya maisha kuwa rahisi watu hawataheshimu fani yako. Hii inapelekea wengi wa wasio wana IT kuogopa na kuona maisha ya huko ni magumu hivyo ni bora waishie kwenye blogu.
Baada ya kuangalia vikwazo, hebu tudokolee nini kifanyike ili kuwasaidia wafanyabiashara wetu?
1. Wanashika dau wa IT wabadili muelekeo
Kuna usemi mmoja unaosema, IT doesnt matter, yaani kuwa na teknohama sio kitu cha ajabu, ila kitu muhimu ni jinsi gani itakavyotumika. katika tafiti zangu, nimegundua kuwa wengi wa washika dau ambao ndio wanategemewa wanakosa kitu kimoja, " Jinsi gani IT itakavyokuwa sehemu ya biashara". Hawa wanatakiwa kuja na mbinu na maarifa ya kuwashawishi wafanyabiashara kubadili mtazamao wao juu ya IT. Hivyo basi elimu ya biashara ni muhimu kwa wna IT kama ilivyo kwa fanni nyingine.
Kwanini ninaongea hivi, kuna kipindi niliwahi kufanya majadiliano na mmoja wa wanablog mkubwa Tanzania, yeye alikuwa anataka kuipeleka blogu yake kwenye hatua ya mbali zaidi kutoka kwenye blogspot. Ila hofu yake ilikuwa, aliwahi kujaribu hapo awali na matokeo yake alipoteza watembeleaji wengi mno, hivyo asingependa hili litokee tena. Hivyo basi shime kwetu wana IT kufikiri nje ya boski, isiwe IT kwa IT, bali IT kwa biashara.
2. Elimu itolewe
Wafanyabiashara hawa wanahitaji elimu ya kutosha juu ya faida za It kwa wao, pia wawe tayari kujaribu na kuzitumia.
Katika baadhi ya China, serikali huwa inaratibu mienendo ya makampuni kadhaa ya It kuona muelekeo wao, serikali hutoa msaada mkubwa kwa makampuni yanayoonekana yana muelekeo mzuri kwenye utendaji haswaa yale ya Wazawa. Kwa mfano, kwa China, mwanafunzi yoyote aliyesoma nje ya Nchi na akarudi kuja kufungua kampuni yake ya IT hupata msamaa wa kodi kwa miaka mitano. Hii huvutia vijana wengi wenye ujuzi kurudi nyumbani hivyo kuleta maarifa na mambo mengi zaidi.
Tawkimu zinaonesha kuwa, hadi sasa kuna Watanzania zaidi ya laki tano wapo nje ya nchi, wengi wao ni nchi zilizoendelea. Ukweli ni kuwa, hakuna binadamu anayependa kuwa muamihaji. Mazingira na hali ya maisha ndiyo yanayowafanya wengi wasirudi nyumbani, hivyo kama Watanzania hawa wakiwekewa mazingira mazuri ya kuwavutia kurudi nyumbani, ni dhahiri wengi wao watarudi kwa makundi.
Wiki ijayo tutaangalia matumizi sahihi ya mitandao jamii kwa biashara.