Jumatatu, 10 Machi 2014 06:45

Makosa 5 ya mawebmaster ya Joomla na jinsi ya kuyaepuka

Written by
Rate this item
(0 votes)

Najua wengi watakuwa wapo excited mno na kutengeneza tovuti zao, ni kweli joomla inarahisisha mambo na kufanya kazi nzima ya utengenezaji wa tovuti kuwa rahisi zaidi. Ila ukweli ni kuwa bado kuna mengi yanatakiwa kufanyika baada ya kutengeneza hiyo tovuti.

Chukulia wewe ni mtengenezaji wa tovuti, baada ya kumaliza kutengeneza tovuti na kumkabidhi mteja wako, wengi wa hawa wateja huwa hawana ufahamu mkubwa wa hii joomla hivyo hufanya mambo mengi mno na kuifanya ile tovuti ambayo wewe ulitengeneza na kujigamba nayo kuwa kimeo na hata kukufanya uikane kama wewe ndiye uliyetengeza. Hii ni kwa sababu wengi wa wanaoanza au kutokuwa na uzoefu wa joomla hufanya makosa mengi kwenye tovuti, hivyo leo nitazungumzia makosa matano ambayo watu hufanya kwenye tovuti za joomla.

Unaweza kusema je Joomla ni kimeo, ukweli ni kuwa, sio kimeo ila urahisi wake unaweza kuwafanya watu wafanye makosa mbalimbali!

Makosa haya ni kutokana na uzoefu wangu binafsi ambao niimepitia hadi kufika hapa nilipo:

1. Linki za tovuti za nje zinafunguka ndani.

Linki za nje ni zile linki za tovuti nyingine ambazo zipo kwenye tovuti yako. Kwa mfano unaweza kuweka linki za partners, ila wengi wetu tumekuwa tukiweka hizi linki kufunguka ndani na kumfanya mtumiaji kupoteza kurasa aliyokuwepo. Hii sio tu inakera bali pia inaweza kukufanya upoteze wateja. Hivyo kumbuka kila unapoweka linki za website za nje, kumbuka kuchagua zifunguke nje.

 

2. Majina ya mafaili yawe yanajieleza.

Chukulia mfano unataka kuupload picha mpya ya gari kwenye tovuti yako, sasa kuna wale ambao wanapenda kurahisisha mambo, wanaweza kuiita 1.jpg, hebu chukulia kesho unataka kubalisha hii picha na nyingine, je utajuaje kama ile 1.jpg ndio picha halisi?? Pia kwa ajili ya kuongeza umaarufu kwenye mitandao (SEO) unashauriwa kutumia majina yenye maana na kueleweka.

3. Kutopunguza ukubwa wa picha.

Moja ya tatizo la joomla ni kutokuwa na uwezo wa kuounguza (resize) ukubwa wa picha yenyewe, wengi wamekuwa wakiupload picha kubwa na kutegemea HTML kurekjebisha ukubwa wa picha, hii ni sawa na itakufanya upate ukubwa kama unaoutaka ila tatizo ni kuwa picha kubwa uifanya website kuwa slow kufunguka. Hivyo ili kurahisisha na kuongeza spidi ya tovuti yako unashauriwa kuupload picha ambazo zina ukubwa unaotakiwa, kwa mfano kama picha inayooonekana ni 30px, basi unaweza kutumia programu kama Photoshop kuresize kuwa 30px na kuipoandisha ikiwa ndogo. Pia usisahau kusave kama picha ya website.

4. Kuandika makala moja kwa moja kwenye joomla.

Kila unapologin kwenye kurasa ya admin ya joomla, unapewa dakika 15 kabla joomla haijakutimua (session off). Kwa kawaida huu muda hauwezi kuubadilisha kwa kutumia ukurasa wa nyuma wa admin (global configuration). Sasa kwa wale wenzangu na mimi wanaoandika magazeti tena kwa kudonoa, utajikuta unapoteza kila kitu tena baada ya kazi kubwa. Hivyo unashauria kutumia Notepad (na sio Microsoft word) kuandika makala yako na kuipaste pindi umalizapo. Nimegusia kutotumia word kwakuwa word huifanya document kuwa na code nyingi na zilizo chafu kitu kinachoweza kupelekea google kutoirank vyematovuti yako. Kumbuka google inapenda sana code safi.

5. Kuweka picha zote sehemu moja.

Uzuri wa joomla ni jinsi gani inavyokuwezesha kucheza na kubadilisha mafaili yaliyo ndani, kwenye joomla picha za makala huwekwa kwenye faili linaloitwa "images", sasa chukulia wewe unatengeneza tovuti ya habari ambapo una makundi mengi, kama kila kitu utaweza humo, je kazi itakuwaje baada ya mwaka mmoja? Unashauri kutengeneza mafaili kulingana na kitu husika, kwa mfano mimi tovuti yangu ya habari ina news, sports... hivyo ninaweza kutengeneza faili kwa kila kipengele na kuupload kila picha kwenye faili husika kulingana na aina yake.

Hayo ndio ambayo ningependa kuwashauri wale wanaoanza au kwa wale wanaotaka kujua zaidi. Je wewe ni webdesigner na umekutana na makosa fulani au ushauri kwa mawebmaster??

Ngaranyiza

Mtumizi wa Joomla! myaka mingi iliopita

www.att-center.de