Hassan Ayeko
Hassan ni mtaalamu wa masuala ya IT pia ni mkalimani mkuu wa Joomla Kiswahili (Joomla Coordinator for Swahili language)
Je bado unatumia Joomla 1.5? Ni muda wa kusasisha (upgrade) sasa!
Katika makala zangu zilizopita, nimeongelea umuhimu wa kusasisha (asante Kaka Hassan kwa kuniongezea msamiati mwingine), sio tu utaongeza ufanisi na usalama wa wavuti yako, bali pia itakuwezesha kuhakikisha unakuwa na wavuti salama na iliyo bora. Ingawa mengi yameiongelewa, mengi yameandikwa, lakini ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu bado tunatumia Joomla 1.5.
Je nitumie Joomla 2.5 au 3?
Nimekuwa nikipokea email na hata simu toka kwa baadhi ya wateja wangu au watu mbalimbali ambao wamekuwa wakisoma makala au kuangalia mafundisho yangu.Moja ya swali ambalo limekuwa likijirudia ni kuwa, tayari Joomla 3 imeshatoka, je kwanini nisiende moja kwa moja hadi Joomla 3 badala ya 2.5? Ili kujibu swali hili kuna mambo kadhaa inabidi kuzingatia.