Usalama na utulivu ni vitu muhimu sana vya kukumbuka ikiwa unaendesha wavuti wa kibiashara. Unatakiwa kuweka programu ya wavuti wako kisasa na kiusalama. Kwa ukweli, unashauriwa kuhakikisha kuwa programu yoyote unayotumia iwe kisasa na kiusalama - ni njia nzuri. Kwa hivi iweke akilini, unashauriwa kusasisha kwa toleo la sasa, kwa sababu matoleo yana viraka vya usalama na maboreshaji, na pia vipengele vipya.
Mfululizo wa Joomla 3.x umepata maendeleo mengi ya usalama, kama vile:
• BCrypt kwa kuvuruga manenosiri
• Uthibitishaji wa kanuni mbili
• 'Nikumbuke mimi' imesitawishwa
Kuanzia toleo 3.2, Joomla imechukua hatua kubwa sana na mawazo mazuri sana, kwa mfano uthibitshaji wa kanuni mbili ulio ndani ya kiini. Toleo 3.3 ni hatua nyingine zaidi.
Kuanzia Joomla 3.3, toleo la chini la PHP linalohitajika kwa kutumia Joomla! ni 5.3.10. Hii inapeana maongezo zaidi ya usalama, pamoja na usimbaji ficha wa manenosiri, na inalinda matatizo yanayosababishwa na mazingira magumu ambayo yanaweza kugonganishwa na matoleo yaliopita ya PHP.
Maboreshaji haya yote ya Joomla yanakupa sababu zaidi kwa kuhakikisha kuwa wavuti wako ni wa kisasa na wa kiusalama - hii utakusaidia wewe kufanya mengi na Joomla!