Print this page
Jumanne, 06 Mai 2014 14:25

Sasisha kwa Joomla! 3.3

Written by
Rate this item
(0 votes)

Joomla! inatangaza matoleo yafuatayo 3.2.4 na 3.3.

Ikiwa kwa sasa unatumia Joomla! 3.2 katika seva ya PHP 5.3.10 au juu, unashauriwa usasishe Joomla! 3.3 upesi kulingana na nafasi yako. Ukitumia utaratibu huu, unashauriwa utumie kipengele cha kusasisha katika upande wa nyuma wa wavuti wako, au ushushe kutoka kwa http://www.joomla.org/download.html.

Kwa wavuti walio na PHP chini ya toleo 5.3.10, nilazima watumie Joomla 3.2.4.

Ni mapya gani kwa Joomla! 3.3?

USALAMA IMARA

Joomla 3.3 inaongeza kiwango cha usalama kwa kufanya PHP 5.3.10 toleo la chini linalohitajika kwa kutumia Joomla! pamoja na usimbaji ficha wa manenosiri.

API KWA KUHIFADHI KATIKA CLOUD

Joomla ni inayofaa kwa mahuduma ya kuhifadhi katika cloud, kama vile Amazon S3, Google Cloud Storage, Rackspace na Dropbox.

KURASA ZA KASI SANA

Mkurugenzi wa trafiki, ambaye anasimamia mawakilishi ya kurasa zote, URL, na kadhalika, sasa ni 10% zaidi kwa kasi - tumia tu matayarisho ya difoti.

JQUERY

Joomla sasa ina maktaba ya JQuery kama sehemu ya kiini. Hii inamaanisha kuwa unaweza kusambaza wavuti walio hawana matatizo ya kiufundi na walio imara sana, na utapunguza muda na gharama za tiketi za misaada.

SEO MICRODATA

Maktaba mapya ya microdata yanaboresha uwezo wa majuhudi yako ya masoko, na inaruhusu kuchukua faida za mabadilisho ya karibuni katika mamashini maarufu ya kutafuta.

Hassan Ayeko

Hassan ni mtaalamu wa masuala ya IT pia ni mkalimani mkuu wa Joomla Kiswahili (Joomla Coordinator for Swahili language)

www.att-center.de

Latest from Hassan Ayeko