Print this page
Ijumaa, 14 Machi 2014 07:20

Mazingatio juu ya kuchagua wapi pa kuweka tovuti

Written by
Rate this item
(0 votes)

Katika miaka ya tisini,tovuti ilikuwa ni kwa ajili ya kusomea barua pepe,kipindi hicho ukiwa na barua pepe basi wewe unaonekana ni bingwa na mtaalam.Maendeleo hayo ya tovuti kwa nyumbani yaliendelea kuwa ni anasa mpaka miaka ya karibuni ambako kwa kasi ya ajabu mambo yamebadilika na kubadilisha uelekeo wa upepo. Ili kuweka mambo sawa zaidi,tuifananaishe tovuti na nyumba,kwani ndani ya tovuti ndipo hazina yako inapokaa kama sisi tunavyokaa kwenye nyumba,unapozungumzia nyumba,kuna makundi mengi,kuna wale wenye nyumba binafsi na wale walioamua kupanga,tovuti nayo vilevile. Leo hii nitakufafanulia kwa undani ni mambo gani unatakiwa kuzingatia kipindi unachagua wapi pa kuweka hazina yako,tutaangalia sana kikazi na kukufanya ujue nini unatakiwa kufahamu ili kuhakikisha unakuwa na tovuti imara na isiyosumbua au kukutia aibu.

Katika ulimwengu wa watoa huduma za kuweka tovuti,kuna machaguo mawili.Moja likiwa ni lile la bure na lingine ni kwa lile la kulipia.haijalishi umeamua kuchagua aina gani,kila kundi kuna mambo mengi ambayo unatakiwa kuzingatia.Tutaanza na zile huduma za bure…

Huduma za bure: Pindi unapoamua kuchagua huduma ya bure,kuna mambo kadhaa unatakiwa kuzingatia kwani katika uwanja wa bashara hakuna kitu cha bure,hivyo tuangalie mambo gani unatakiwa kuzingatia.

 

1. Matangazo

Kama nilivyokwisha dokeza,hakuna kitu cha bure kwenye dunia hii,hivyo hawa jamaa wanaotoa hizi gharama za bure,huweka matangazo kwenye tovuti ili kufidia gharama za uendeshaji.Kumbuka kuwa kuna baadhi ya matangazo hukera mno watembeleaji,kwa mfano yale yanayojitokeza kwa kupop na kumfanya mtumiaji kushindwa fanya lolote kitu kinachompelekea kuondoa.Pia kuna maswala ya mila na desturi.Kwa mfano chukulia hao jamaa wanaotoa hizo huduma ni wachina au wajapan,sasa kule kwao kuna baadhi ya maneno ambapo kwao ni mazuri ila hapa kwetu ni lugha mbaya.

Vilevile,ukija kwa upande wa kiufundi,huduma hizi huweza kuathiri upatikanaji wako kwenye mitandao ya utafutaji(SEO),hivyo wewe kama mtunza tovuti inabidi utafakari kwa undani kabla hujafikia maamuzi.

 

2. Kiasi cha kujinafasi

Nyingi ya hizi huduma za bure hutoa kiasi ambacho kinakuwa na ukingo,kwa mfano wengi wao hukupa 5MB,je kiasi hicho kinakutosha? Kwa tovuti yabisi(static website) hili linaweza lisewe tatizo,ila kama unataka tovuti inayojiongoza(dynamic) 5MB sio kitu.

Katika suala la nafasi,pia unatakiwa kuzingatia ukuaji(scallability),hapa ninamaanisha endapo kwa siku za usoni umeona nafasi haitoshi na kuamua kuongeza nafasi zaidi,je gharama inakuwaje? kwani katika vitu vinavyokera ni kuhamisha tovuti toka seva moja hadi nyingi,hakikisha unapata seva ambayo ina mpangilio mzuri wa ukuaji.

 

3. Matumizi ya FTP

kama umeshawahi kuwa na tovuti,basi FTP ni kitu cha msingi kukifahamu,Sio tu kuwa moja ya roho za tovuti bali pia ni moja ya vitu inavyoweza kukurahisishia kazi kwa kasi ya ziada.FTP itakuwezesha kutuma na kupokea mafaili makubwa toka kwenye tovuti yako,kitu ambacho ni muhimu haswa wakati unatengeneza au kuirusha tovuti.

 

4. Viwango vya utumaji

Kuna baadhi ya watoa huduma huweka vizingiti kwa kiwango gani unaweza kutuma na kupokea,sio tu kwa ukubwa bali huweza kuja kwenye aina ya faili unaloweza kutuma na kupokea.Kwa mfano kuna baadhi ya watoa huduma huruhusu utumaji wa picha zilizo kwenye mfumo wa jpg na sio gif.Hivyo kama unataka kuweka mifumo mingine inabidi kuongeza gharama za ziada au kutafuta mtoa huduma nyingine.

 

5. Upatikanaji

Kipindi naingia kwenye ulimwengu wa tovuti,nilipata maumivu ya kichwa yasiyo n kikomo,kwani ile seva ambayo nilikuwa natumia kila siku jioni ilikuwa inajizima(haipatokani),ukizingatia muda huo kwa hapa watu wengi ndio wapo nyumbani wanataka kuitembelea tovuti.Utata ukaja kuwa kwakuwa nilikuwa natumia huduma ya bure,hivyo maswali(matatizo yangu hayakupewa kipaombele).

Hivyo ni kati ya vitu vya msingi ambavyo unatakiwa kuzingatia pindi unachagua huduma ya bure,kumbuka huduma hizi nyingi huwa na gharama zilizojificha nyuma yake,mfano kutunza tovuti ni bure ila kama unataka msaada wa utatuzi wa matatizo inabidi ulipie kitu ambacho siku ya mwisho unajikuta unalipia gharama sawa na kama ungelipia.Ila kuna wengine ambao wanatoa huduma nzuri ilihali wameweka matangazo yao.

 

Sehemu ya pili tutaangalia huduma za kulipia.

Ngaranyiza

Mtumizi wa Joomla! myaka mingi iliopita

www.att-center.de

Latest from Ngaranyiza