Print this page
Jumatatu, 10 Machi 2014 04:20

Mazingatio ya usalama wa joomla kwa mawebmaster Joomla (wanaoanza)

Written by
Rate this item
(0 votes)

Siku si nyinzi zilizopita tumeanza kutoa mafundisho ya matumizi ya joomla, ni dhahiri kuna watu wengi wamepata na mori na kuanza kutumia joomla. Pia jana katika pitapita zangu tena katika tovuti moja ya idara muhimu ya serikali nikaona kuna matangazo ya ajabu mno ya video za kikubwa (hehe), hii ilifanyika bila webmaster kujua. Hivyo ili kuwasaidia mawebmaster wanaoanza, leo hii tuangalie mambo machache ambayo wewe kama webmaster wa joomla unatakiwa kuzingatia. Kumbuka haya ni mazingatio muhimu ambayo unatakiwa kuzingatia kabla ya kuweka tovuti yako online.

 

 

1. Backup backup backup

Ukweli ni kuwa website yoyote inaweza kuvamiwa na hackers, hakuna ubishi kwenye hili, hivyo kitu cha msingi ni kujiandaa ili pindi pale uvamizi utakapotokea basi angalau una pa kuanzia. Tunashauri kutumia Akeebabackupkwenye hili. Kumbuka kuwa unatakiwa kufanya backup kila kunapokuwa na vitu vipya hivyo uamuzi ni wako wa ni jinsi gani na lini utafanya hii backup. Akeeba inakuwezesha kufanya backup ya website nzima au kwa database tuu.

 

2. Tumia toleo jipya

Nimewahi kutembelea tovuti nyingi mno tena ni za muhimu mno na kuwakuta bado wanatumia matoleo ya zamani ya joomla, hii sio tu inawafanya waonekani sio makini bali pia inawafanya wawe nje nje na uvamizi. Kumbuka joomla hutoa maboresho (updates) kila kipindi pindi tuu panapogundulika mwanya kwenye sehemu fulani ya program yao. Ili kufahamu hili pia unashauriwa kujiunga na milisho(updates feeds) toka Joomla.

 

3. Zuia joomla backend

Wewe nenda kwenye tovuti nyingi na uandike www.jinalatovuti.com/administrator na utajikuta upo sehemu ya admin, jaribu kupunguza urahisi wa kuvamiwa kwani kwa kufanya hivi, mahacker wataingia kwa urahisi kwa kujaribu password kadri wawezavyo.

 

4. Badili jina la admin na ID yake

Kwa mara ya kwanza kwenye tovuti ya joomla, super user ni admin na namba yake (ID) ni 42 kwa joomla 2.5, hivyo kwa kufahamu taarifa hizi, mvamizi anaweza kuzitumia kuvamia tovuti yako. Hivyo inashauri ubadilishe au hata kuifuta akaunti ya admin. Ila kumbuka kabla ya kuifuta unatakiwa kutengeneza akaunti nyingine na uipe ruhusa za admin. Ahsante kuna programu moja inaitwa Admin tools inaweza kufanya hili kwa kubadilisha ID ya admin bila utata.

 

6. Epuka extensio zisizo za lazima

Ni kweli pindi unapoanza kutengeneza tovuti ya joomla utakuwa exited na kila extension, kwako wewe kila extension ni bomba, kuna extensions nyingi mno ambapo sio salama au zimetengenezwa hovyo na zinaweza kuhatarisha usalama wa tovuti yako. Hivyo chagua zile programu zinazokubalika kwa ubora haswaa zilizo kwenye oorodha ya joomla (Extension Directory) pia usisahau kuangalia extensio zote zenye mianya ya kiusalama huwa zinaorodheshwa hapa.

 

Tukutane sehemu ionayofuata kwa watumia wa kati na juu

Ngaranyiza

Mtumizi wa Joomla! myaka mingi iliopita

www.att-center.de

Latest from Ngaranyiza